Pages

Saturday, April 27, 2013

CRDB yakarabati wodi Hospitali ya Moro.

UKARABATI wa wodi namba sita katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro uliofanywa na Benki ya CRDB umegharimu sh milioni 50.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema jana kuwa fedha zilizotumika kufanya ukarabati huo ni kutoka katika akaunti ya watoto ya Junior Jumbo iliyopo katika benki hiyo na kwamba iliamua kufanya ukarabati huo baada ya kuona ubovu wa wodi hiyo.
Alisema benki hiyo imekuwa na vipaumbele vyake katika kuchangia masuala mbalimbali ya kijamii hasa katika masuala ya afya, elimu na mazingira.

“CRDB imekuwa ikilipa kodi kubwa, tena bila kuchakachua na kila mwaka tumekuwa tukilipa sh bilioni moja, jambo ambalo tunajivunia,” alisema Dk. Kimei.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi, akizindua wodi hiyo aliipongeza CRDB kwa uamuzi wa kuifanyia ukarabati wodi hiyo na kuyataka mashirika na taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Pia aliwataka wananchi hasa watumiaji wa wodi hiyo kutunza miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na vifaa.

No comments:

Post a Comment