Pages

Tuesday, April 30, 2013

DC ashauri wanawake kuunda vikundi.

Mkinga. Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza amewataka wanawake wa Mkinga kuunda vikundi vya ushirika, ili kuweza kujikwamua na maisha pamoja na kuimarisha biashara zao na kuacha kukaa nyumbani.
 
Akizungumza katika mafunzo na wanachama wa Vikoba wa Maramba na kufadhiliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mgaza alisema siri ya kutoka katika dimbwi la umaskini ni kujishughulisha na kazi za ujasiriamali. 

Alisema wilaya hiyo yenye mwambao wa bahari pamoja na ardhi nzuri ya kilimo cha mbogamboga na matunda ni fursa tosha kwa wajasiriamali wa kike na kiume kubuni mbinu mbadala za kujikwamua na umaskini.
 
Alisema kutokana na ufunguzi wa barabara mpya ya kiwango cha Lami Tanga, Horohoro, ni wakati wa wafanyabiashara wakubwa na wajasiriamali kutafuta masoko ya bidhaa zao katika masoko yaliyoko ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Akizungumza katika mafunzo hayo, Mshauri Elekezi wa Masuala ya Ujasiriamali TPSF, Jane Gonsalves,alisema sekta hiyo ilifanya uchunguzi katika wilaya hiyo na kugundua wajasiriamali hawana elimu ya biashara (Salim Mohammed)

No comments:

Post a Comment