Pages

Monday, April 29, 2013

KASHIFA HAIMTOI MSANII – MARIAM ISMAIL.

MARIAM Ismail mwigizaji wa filamu anasema kuwa umaarufu kwa msanii si lazima ajengwe kwa kuandikwa kashifa katika vyombo vya habari bali ni kuitendea haki filamu anayochaguliwa kama ambavyo yeye anaamini anafanya hivyo katika filamu anazocheza kila anapochaguliwa jambo ambalo hivi sasa kila mtayarishaji anahitaji kufanya kazi naye kwa sababu anajua.
                                             Mariam akiwa katika pozi la kikazi.
“Binafsi sihitaji scandle ili niwe maarufu bali ninachofahamu ni uwajibikaji katika kazi ninayopewa na mtayarishaji wa filamu husika, ninachohitaji ni kusoma muswada wa filamu (Script) vizuri kisha
kuvaa uhusika kulinga na nafasi nitakayopewa kuigiza mara nyingi wasanii tunahitaji hisia, hicho ndicho ninachofanya katika filamu zote nilizoigiza na kunifanya niwe bora,”anatamba Mariamu.
Msanii huyo ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahiliwood ameshiriki katika filamu
Endelea kusoma kwa kubofya...Read more..
Best Man, Wrong decision, Iddentical, Samatha, Doa la Ndoa na filamu nyingine msani huyo ni zao la Mtitu kutoka 5 Effect ambaye mara nyingi ukuza vipaji vya
filamu Bongo, Mariam anafananishwa na mwigizaji wa kike wa Nigeria Omotola Jilade lakini mwenyewe anadai anamhusudu sana msanii Kemmy.

No comments:

Post a Comment