Pages

Friday, April 26, 2013

KATAIKA KUPUNGUZA FOLENI SERIKALI IMETIA SAINI KWA AJILI YA UJENZI WA KIVUKO.

Katika kupunguza tatizo la Msongamano wa Magari jijini Dar es Salaam Serikali kupitia Wizara ya ujenzi imetia saini ujenzi wa kivuko kipya cha kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo kitachokiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 300 kwa wakati mmoja.
 
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko hicho kitakachojengwa kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark Waziri wa Ujenzi Dokta JOHN MAGUFULI amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni utekeleaji wa ahadi zilizotolewa na Rais JAKAYA KIKWETE wakati wa kampeni za uchaguzi za Mwaka 2010 sambamba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2005.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam SAID MECKY SADICK ameelezea namna kivuko hicho kitakavyosaidia kupunguza tatizo la msongamano wa magari.

No comments:

Post a Comment