Pages

Thursday, April 25, 2013

Kikwete aombwa kuingilia mgogoro Kurasini Wilaya ya Temeke

RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kuingilia kati mgogoro wa wakazi wa Kata ya Kurasini,  Wilaya ya Temeke na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo inataka kuwahamisha kinyume cha sheria.

Akizungumza juzi, kiongozi wa wakazi hao zaidi ya 2,000, Gustavu Mihanjo alisema wanashangazwa na uamuzi wa wizara kudharau amri ya mahakama inayowataka kusimamisha bomoabomoa ya nyumba za wakazi hao.
Alisema wataridhika endapo Rais Kikwete atafika katika eneo hilo ili waweze kumueleza vitendo viovu wanavyofanyiwa na watendaji wake.

“Tunamuomba rais aje mwenyewe Kurasini na kutupa nasaha. Sisi wananchi tutaridhika kama atakuja yeye mwenyewe na sio kutuma ujumbe.
“Pia tunaomba hawa wanaovunja amri ya mahakama wachukuliwe hatua kali kwa sababu sasa ni mara ya pili wanafanya kitendo hiki,” alisema Mihanjo.

Alisema kuwa maelezo ya Waziri wa Ardhi kuwa eneo lote linatakiwa ili kubadilishwa matumizi lilipaswa kutolewa siku 90 kabla ya kitendo hicho kufanyika.
“Kurasini ni mahala petu pa makazi, bila ya ushauri wowote wanakuja kutuletea amri ya kuvunja nyumba zetu  wakati kesi bado ipo mahakamani,” alisema.

No comments:

Post a Comment