Pages

Tuesday, April 30, 2013

Marais EAC watangaza mikakati ya uchumi bora.

Arusha.  
Mataifa ya Afrika ya Mashariki (EAC), yamekubaliana kuwa na mkakati wa pamoja kwa kukuza uchumi, kwa kutumia rasilimali ambazo zimegundulika katika nchi  hizo kama mafuta, gesi na madini.



Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kushoto) na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Arusha jana. Picha na Filbert Rweyemamu

Mwenyekiti wa Marais wa nchi za Afrika ya Mashariki, Yoweri  Museven aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa  11 wa wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki uliofanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto mkoani hapa.


Rais Museven alisema, rasilimali zilizogundulika sasa katika nchi za Afrika ya Mashariki, zikitumiwa vizuri zinaweza kuzifanya  nchi zote za Afrika ya Mashariki kutoka katika nchi zinazoendelea kuwa nchi zilizoendelea ifikapo mwaka 2063.


Awali, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema nchi za Afrika Mashariki, pia zinaweza kuendelea kwa kasi, kama zikifufua mipango ya pamoja ya kuboresha sekta ya Miundo mbinu, ikiwamo ya  usafiri  wa reli, barabara na bandari.

Kenyatta ambaye jana ilikuwa mara yake ya kwanza kuhutubia kikao cha Marais na 


Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki , kama Rais wa Jamhuri ya Kenya ,alisema  miradi ya pamoja katika nchi za Afrika ya Mashariki, kutasaidia sana kukuza uchumi kwa kasi kwa kila nchi badala ya kila nchi kuendeleza mradi wake.

“Tunahitajika kufanyakazi kwa pamoja katika kuendeleza miradi mbalimbali na hapo ndipo tutawavutia wawekezaji na hivyo kuinua hali ya uchumi”alisema Kinyatta
 

Katika mkutano huo, Marais wanne,waliohudhuria, walijadili   itifaki  ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini  Novemba mwaka huu.

Marais hao,  Museveni wa Uganda, Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pierre Ngurunziza wa BurundI na Uhuru Kenyatta wa Kenya,  pia  waliwaapisha Naibu Katibu Mkuu  wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,kutoka Kenya, Charles Njoroge ambaye anachukuwa nafasi ya Dk Julius Rotich  aliyemaliza muda wake.

Marais hao, pia waliwaapisha  majaji wawili, wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki.

No comments:

Post a Comment