Pages

Tuesday, April 16, 2013

Mke wa Ravalomanana kugombea urais Madagascar.

Rais wa zamani wa Madagascar, Mark Ravalomanana ametangaza kuwa, mke wake Lalao Ravalomanana atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Julai 24.


Lalao ni mwanamke wa 4 kujitosa uwanjani na anatarajiwa kuchuana na vigogo wengine wa kisiasa nchini humo. 

Rais wa sasa Andry Rajoelina aliingia madarakani mwezi Machi mwaka 2009 baada ya kumpindua Mark Ravalomanana. Baada ya hapo, kiongozi huyo aliyepinduliwa alikimbilia uhamishoni Afrika Kusini.

Duru za habari zinaarifu kuwa, uamuzi wa Mark Ravalomanana wa kumpendekeza mke wake kuwania urais, umepata baraka kutoka kwa wapambe wake wa karibu. Hii ni katika hali ambayo, uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Madagascar unaonyesha kuwa, watu wengi wanapendelea nchi iongozwe na rais mwanamke.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, makubaliano ya kutatua hali ya kisiasa ya Madagascar yanamzuia Andry Rajoelina na Mark Ravalomanana kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

No comments:

Post a Comment