Pages

Sunday, April 28, 2013

PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ifunda, Padri Alphonce Mhamilawa, amefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea katika eneo la Sabasaba, Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ifunda, Padri Alphonce Mhamilawa, amefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea katika eneo la Sabasaba, Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda walieleza kuwa ajali hiyo ilitokea saa nane usiku wa kuamkia jana wakati paroko huyo akitoka mkoani Njombe katika shughuli ya mazishi.

Mmoja wa mashuhuda hao, Saugo Ndemo, alisema kuwa paroko huyo alikuwa akiendesha gari dogo aina ya Toyota Hilux (Pick Up) lenye namba za usajili T 434 APP mali ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni paroko kuligonga lori kwa nyuma ambalo hata hivyo halikusimama baada ya ajali hiyo.

Alisema kuwa paroko huyo alikufa pale pale kutokana na kichwa chake kupasuka.

Mmoja wa askari wa usalama barabarani ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji rasmi wa jeshi hilo, alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
 
No comments:

Post a Comment