Pages

Thursday, April 25, 2013

PICHA ZA 4 JENGO LA GHOROFA NANELILILOANGUKA SIKU YA JUMATANO JIJINI DHAKA BANGLADESH ZIKO HAPA.

Matukio ya majengo kuporomoka nchini Bangladesh ni ya kawaida kutokana na majengo mengi marefu kujengwa kinyume na sheria za ujenzi.
Jengo lililoporomoka lilikuwa na kiwanda cha nguo, benki na maduka kadhaa. Liliporomoka asubuhi wakati watu wakielekea makazini.


Watu wengi walikusanyika karibu na eneo la tukio wakiwatafuta ndugu na marafiki. Haijafahamika kilichosababisha jengo hilo kuporomoka, lakini vyombo vya habari nchini humo vimesema kwamba, nyufa zilionekana kwenye jengo hilo siku ya Jumanne.


Polisi wameviambia vyombo vya habari kwamba, waliona ghafla sehemu ya nyuma ya jengo hilo ikianguka Jumatano asubuhi na baada ya muda mfupi jengo lote likafuatia isipokua nguzo kuu na sehemu ya ukuta wa mbele hali iliyosababisha taharuki.

Maafisa wanasema, ni sehemu ya chini pekee ya jengo hilo la Rana Plaza ndio ilibakia imara baada ya kuporomoka, wakati wanajeshi na waokoaji wa idara ya zimamoto wakiwa na vifaa vya kukatia vyuma na matingatinga wakifukua vifusi ili kuwaokoa watu walionaswa .

Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Mohammed Asaduzzaman, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, hali ilikua mbaya sana.

No comments:

Post a Comment