Huko
Nou Camp Mashabiki wakidhani Barcelona watapindua kipigo cha awali cha
4-0 walichopewa na Bayern Munich kwenye Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali
ya UCL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, lakini leo Bayern Munich wameendeleza
kipondo kwa kuibonda tena Barca Bao 3-0 na wao kutinga Fainali
watakayocheza na wenzao Borussia Dortmund.
Full shangwe..
Hii ni Fainali ya 3 kwa Bayern Munich, ambao wako chini ya Kocha Jupp Heynckes ambae mwishoni mwa Msimu anaondoka na Msimu ujao kuja Kocha wa zamani wa Barca Pep Guardiola, kutinga ndani ya Miaka minne

Mwaka jana walitolewa na Chelsea kwa Mikwaju ya Penati tano tano kwenye Fainali iliyochezwa huko Allianz Arena Mjini Munich ambako ndio Uwanja wa Nyumbani wa Bayern Munich.

Lionel Messi hakucheza, alibaki Benchi, na bila ya yeye, baadhi ya Wadau hunena ni sawa na QPR na leo ndani ya Uwanja wao Nou Camp hilo limedhihirika kwa kuwafuata wenzao Real Madrid ambao jana walibwagwa nje na Borussia Dortmund.



Wakijiuliza kipi kilichowasibu... Gerard Pique, David Villa na Cesc Fabregas ili wakitibu haraka

Marc Bartra akianguka chini na aliyesimama ni mchezaji Mario Mandzukic






Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer (kushoto)kwa furaha zao kuelekea Fainali itakayofanyika tarehe
25 Mei 2013 UWANJA wa WEMBLEY, London.

VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra (Montoya 87), Adriano, Xavi (Sanchez 55), Song, Iniesta (Thiago 64), Villa, Fabregas, Pedro.
Subs not used: Pinto, Messi, Jonathan, Montoya, Tello.
Booked: Dani Alves
Bayern Munich: Neuer, Lahm (Rafinha 77), Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi Martinez (Tymoschuk 74), Schweinsteiger, (Gustavo 66) Robben, Muller, Ribery, Mandzukic.
Subs not used: Starke, Dante, Shaqiri,Gomez.
Goals: Robben 49, Pique o.g. 72, Muller 76
Booked: Robben
Referee: Damir Skomina (Slovenia)
No comments:
Post a Comment