Pages

Thursday, May 9, 2013

KITUKO... SHIJA ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE WA WANYAMA.



Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Deogratius Shija ametoa kali ya mwaka baada ya kusema anajiandaa kugombea ubunge kwa nia ya  kutetea haki za wanyama kwani hawana mtetezi bungeni.
 
Akichonga na paparazi wetu, Shija alisema mwaka 2015 kutokana na kwamba kutakuwepo na katiba mpya atagombea ubunge kama mgombea binafsi kwa ajili ya kwenda kuwatetea wanyama hao ambao mpaka leo hakuna anayewatetea.
 
“Nina mpango wa kugombea ubunge kwa ajili ya kuwatetea wanyama kama paka, mbwa, ng’ombe, punda na wengine wengi kwani nimegundua binadamu wanawatesa sana na hawana mtu wa kuwatetea.
 
“Wazo hili nililipata mwaka jana nilipotembelea nchi ya Kenya nikakuta kuna wabunge wa kutetea haki za wanyama hivyo hapa Tanzania katiba hiyo ikipita naamini na mimi  nitakanyaga bungeni,” alisema Shija.

No comments:

Post a Comment