Pages

Monday, May 13, 2013

Kumekucha Redd’s Miss IFM kufanyika katika Hoteli ya JB Bellmonte Posta Mpya, Dar es Salaam.


KILE kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss IFM sasa kimefikia patamu ambako warembo 10 bomba watapanda jukwaani katika kuwania taji hilo Mei 25, kumsaka mrithi wa mrembo atakayevua taji hilo Fina Revocatus.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Hoteli ya JB Bellmonte iliyopo Jengo la Golden Jubilee, maeneo ya Posta Mpya, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Redd’s Miss IFM, Daniel Sarungi alisema mshindi wa taji hilo ataondoka na kitita cha sh mil.1.
“Warembo 10 ndio watakaoshiriki katika shindano hilo na mshindi ataondoka na sh mil 1, huku washindi wengine watatu tukitarajia kuwapa zawadi nyingine nzuri zaidi,” alisema Sarungi.
Meneja wa Redd’s Original ambao ni wadhamini wakuu wa Redd’s Miss Tanzania, Victoria Kimaro alisema wanajivunia kuwa sehemu ya udhamini wa shindano hilo na wanaamini warembo hao watafanya kweli zaidi na kutwaa taji la Miss Tanzania.
“Hili shindano la Redds Miss IFM  litakuwa moto, kwani tutalipa sapoti kubwa zaidi na kuhakikisha anatoka mrembo atakayetwaa taji la Redd’s Miss Tanzania,” alisema Victoria.

No comments:

Post a Comment