Pages

Tuesday, May 14, 2013

Mnigeria akamatwa Kia na ‘unga’

Moshi.
Vyombo vya ulinzi na usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), vimemtia mbaroni raia wa Nigeria akiwa amebeba kilo saba za dawa zinazoaminika ni za kulevya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema raia huyo wa Nigeria alikamatwa saa 8:00 usiku wa kuamkia juzi, akijiandaa kuingia katika jengo la uwanja huo.
Boaz alisema mtuhumiwa huyo ambaye amejitambulisha kuwa ni mfanyabiashara, alikuwa asafiri kwenda Ouagadougou kupitia Adiss Ababa kwa ndege ya Shirika la Ethiopian Airline.

“Wakati anaingia pale uwanjani alipekuliwa na kukutwa na kilo saba za dawa za kulevya zikiwa zimefichwa katika mabegi yake manne ya kusafirikia,” alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema uchunguzi wa kina kubaini aina ya dawa hizo unaendelea, lakini uchunguzi wa awali unaonyesha unga huo ni dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment