Pages

Friday, May 10, 2013

Redds Miss Singida Mei 31,2013.

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Mkoa wa Singida, Redds Miss Singida 2013 linatarajiwa kufanyika Mei 31 mjini hapa.
 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Mratibu wa Miss Singida, Aunt Borah alisema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yanaendelea vizuri.
Alisema shindano hilo mwaka huu limeboreshwa ikilinganishwa na ya miaka ya nyuma na kwamba warembo wanamiminika kuchukua fomu za ushiriki.

Aidha, Aunt Bora alisema warembo nane kutoka Singida Mjini tayari wameishachukua fomu na baadhi walishajaza na kuzirejesha, pia warembo watatu kutoka Chuo cha Uhasibu tawi la Singida nao wamechukua fomu za ushiriki.
“Shindano wa kumsaka mrembo wa Wilaya ya Iramba limeishafanyika na warembo walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu, watashiriki shindano la mkoa… lakini kwa sasa naomba nisitoe majina yao, ila nitafanya hivyo wakati ukifika,” alisema na kuongeza:

“Nitumie tu nafasi hii kuwaomba warembo zaidi waendelee kujitokeza kujaza fomu, ili kutengeneza mazingira ya kuwa na ushindani wa kweli utakaotoa washindi ambao watafanya vizuri mbele ya safari.”

Katika hatua nyingine, Aunt Borah ambaye pia anamiliki saluni maarufu mjini hapa ya Aunt Borah, alisema kwamba kuna wadau wameonesha nia ya kuwa wadhamini wa shindano la mwaka huu na bado nafasi ipo kwa wengine zaidi kujitokeza.

No comments:

Post a Comment