Pages

Sunday, June 23, 2013

Auawa siku moja baada ya kutoa ushahidi

MKAZI wa Kijiji cha Stalike, wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi, Thobias Amando  (54), ameuawa kwa kushambuliwa na watu wasiofahamika.
Amando aliuawa siku moja baada ya kuwa shahidi katika mauzo ya shamba kati ya muuzaji, Sadoti  Tende na  mnunuzi, Gasper Damian. Shughuli ya mauziano ya shamba hilo ilifanyika  nyumbani kwa  Gasper.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi, Emmanuel  Nley,  alisema mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia juzi kijijini hapo.
“Siku moja  kabla ya  tukio  marehemu  alifuatwa nyumbani kwake  na jirani yake ili akawe shahidi   katika mauziano ya shamba  kati ya Sadoti  Tende ambaye alikuwa muuzaji na  Gasper Damian  kama mnunuzi wa shamba hilo,  mauziano hayo yalifanyika nyumbani kwa  Gasper Damian,” alisema.


Baada ya hapo  marehemu hakurejea nyumbani  kwake  hadi kesho yake  majira ya saa tano asubuhi  ambapo mkewe, Magreth Kaombwe,  aliamua  kwenda kumfuatilia nyumbani kwa Gasper baada ya kuona mumewe hajaonekana nyumbani,” alisema kamanda huyo wa Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mke huyo wa marehemu alipofika nyumbani kwa Gasper  alimkuta na alipomuuliza mumewe yuko wapi, Gasper alijibu tangu walipoachana jana baada ya kumaliza shughuli ya kuuza shamba  hajaonana naye.
Alisema mwili wa marehemu ulikutwa kichakani na watu wawili waliohusika na mauzo ya shamba hilo, Gasper  na   Damian wanashikiliwa na polisi.

No comments:

Post a Comment