Pages

Saturday, June 1, 2013

BASATA yatoa salamu kifo cha Ngwair.

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeelezea kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya muziki nchini, Albert Mangwea ‘Ngwair’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, baraza limeshtushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo cha Ngwair, ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.

Materego alisema baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
“Tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu,” alisema Materego.

No comments:

Post a Comment