BINTI ANUSURIKA KUNYONGWA NA MUMEWE AMBAYE NI ASKARI MPELELEZI HUKO IRINGA.
Hapa
Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari
huyoHapa akionekana mwenye uvimbe zaidiHapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyoHapa akiwa hoi kwa kipigo
Bi Rehema Shauri Madongo mkazi wa Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto
wake baada ya kuponea katika tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo kutoka
kwa mmewe ambaye ni askari polisi mjini Iringa kiasi cha kukimbia nyumba
na kurudi kwa wazazi wake
stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye
amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye
anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa
na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote
zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .
" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha
upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza
kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa
nikiyapata"
Anasema kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume
wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo
zimetoka kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo
kikali. Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo
hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .
Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya
zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika
kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi
ndani ya nyumba.
" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa
nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali
kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi
nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku
nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi
mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo
amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi
kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili
wa kinyama. Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali
ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na
kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua .
Alisema kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume
huyo alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi
ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto. Aidha
alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji
unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari
polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist
Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa
amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake
ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya
RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika
kulishughulikia suala lake Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani
kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi
wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi
wake .
Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .Kwa upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa
amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo
amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.
Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa
wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia
ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa
akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja
mauti.
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana
na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa
sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo
aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama
kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa
Iringa ila askari wenzake wanamlinda.
Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema
anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari
kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili
kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.
No comments:
Post a Comment