Pages

Wednesday, June 26, 2013

SHAMSA: SITAKI KUFUNGA NDOA, ITANISHINDA

MSANII wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa anajuta kukimbilia kuishi na mwanaume kabla ya kufunga ndoa hali inayomfanya aogope  kuolewa kwa kuhofia kushindwa maisha hayo.
Shamsa Ford.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shamsa alisema amekuwa akitamani kuishi bila ya mwanaume tofauti na anavyoishi na mchumba wake wa muda mrefu, Dick.
“Yaani sikufichi kabisa, najuta kwa nini nilikimbilia kuishi na mwanaume kabla ya kufunga ndoa maana hivi sasa nimeshachoka na natamani kuishi peke yangu,” alisema.
 
Kutokana na hali hiyo, msanii huyo amesema ndiyo maana amekuwa akikwepa kufunga ndoa na mwanaume huyo aliyezaa naye mtoto mmoja kutokana na kuchoka kuishi pamoja kwa kuhofia misukosuko ya ndoa.
 
“Naogopa hata kufunga ndoa kwa kuwa nimeshachoka kuishi na mwanaume, sasa nikifunga ndoa naona kama vile itanishinda mapema,” alisema Shamsa.
Via GLP

No comments:

Post a Comment