Pages

Sunday, July 28, 2013

Bibi Bomba kuchujwa kuwapata mabibi 10 wa kuingia katika nyumba ya mwaka huu.

WASHIRIKI 20 wa shindano la kumtafuta ‘Bibi Bomba’ wa mwaka 2013, wanatarajia kuchujwa rasmi kuwapata mabibi 10 wa kuingia katika nyumba ya mwaka huu Mbezi, baada ya mfungo wa Ramadhani.

Mabibi hao 20 waliingia kambini rasmi baada ya kupigiwa kura na wapenzi wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka tangu mwaka jana, jijini Dar es Salaam kupitia televisheni ya Clouds.


Mratibu wa shindano hilo, Lee Ahmed,  alisema jana kwamba shindano hilo liliwahusisha mabibi 20 kabla ya kuchujwa na kubaki 10, ambao wataendelea kuchujwa hadi siku ya fainali itakayotoa mshindi.

Alisema katika kujenga jamii yenye mapenzi mema na mabibi, mashindano hayo yatarushwa katika televisheni ya Clouds TV na kusema hao 20 walitokana na mabibi 60 waliojitokeza kushiriki kabla ya kuchujwa na kubaki hao.

“Tunategemea mabadiliko makubwa mwaka huu kutokana na kuongezeka idadi ya washiriki ambapo wataendelea kuchujwa kupitia kura za watazamaji wa televisheni, ambapo inaweza kuwa zaidi ya miezi mitatu,” alisema Ahmed.

Alisema mabibi hao wataonesha mapenzi yao ya kucheza muziki kwa swaga za kileo, kupenda kuimba na mbembwe ambazo anaamini vitakuwa kivutio katika shindano hilo linalofanyika chini ya udhamini wa ‘Wazazi Nipendeni’.

No comments:

Post a Comment