Pages

Monday, July 29, 2013

Hatimaye Cesc Fabregas akubali kwenda Manchester United.

Chanzo cha habari cha The Daily express kimeeleza kwamba Cesc Fabregas amekubali kujiunga na Manchester United.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa gumzo baada ya ofa mbili za kumnunua toka kwa Manchester United kukataliwa, lakini sasa mchezaji huyo wa
kimataifa ameonesha dhamira yake kurudi Ligi ya Uingereza.
Wakala wa Fabregas Darren Dein amekutana na makamu mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward na imebainika kwamba Nyota huyo wa zamani wa Arsenal yuko tayari kujiunga na Manchester United msimu ujao.
Fabregas ana furaha na anakubaliana na vigezo vilivyotolewa na Man United na sasa atamsikiliza bosi mpya wa Barcelona Gerardo Martino kama atamruhusu kuondoka Nou Camp, lakini kwa upande wa mchezaji huyo yuko tayari kupeleka maombi ya kuondoka Barca.
Fabregas amefurahia mafanikio aliyopata Barcelona, amefunga mabao 29, pasi zilizozaa magoli 32 na ameichezea klabu hiyo ya Catalan mara 96.

David Moyes anataka kuboresha sehemu ya kiungo kwenye timu yake wakati Paul Scholes akifikia ukingoni na Darren Fletcher akiwa anarudi kwenye hali yake baada ya kuwa majeruhi kwa muda sasa, kocha huyo mpya wa Man U amehusishwa mara kadhaa na nyota wa Everton Marouane Fellaini na Yohan Cabaye wa Newcastle United.

No comments:

Post a Comment