Pages

Wednesday, July 31, 2013

HATIMAYE SERIKALI YAIFUNGA SHULE YA SEKONDARI YA LUTHERAN JOURNIOR YA MJINI MOROGORO BAADA YA WANAFUNZI KUGOMA KWA SIKU TATU.

Mgomo wa wanafunzi zaidi ya 600 wa shule ya sekondari ya seminari ya lutheran journior ya mjini Morogoro wa kutoingia darasani mpaka madai ya kero zao yatatuliwe umeingia hatua mpya baada ya serikali kuchukua hatua ya kuwafukuza wanafunzi wote shuleni hapo na kufunga shule hiyo kwa muda usiofahamika .

Hatua hiyo ya serikali imekuja kufuatia wanafunzi hao kukataa kuzungumza na kumzomea katibu mkuu wa kanisa la kinjiri la kirutheri KKKT Brighton Killewa ambaye alitumwa na askofu wa kanisa hilo nchini Alex Malasusa kusikiliza madai ya wanafunzi hao ambayo ni pamoja na kutaka mkuu wa shule hiyo aondolewa shuleni hao kutokana na kuendesha shule huyo kidikteta pamoja na walimu wanaoajiriwa hapo kutokuwa na sifa hali inayofanya shule kushuka kitaaluma .
 
Kasilda Mgeni Mulimila kutoka Morogoro anataarifa zaidi.......

Huyu ni katibu mkuu KKKT akiwa hana la kufanya baada ya wanafunzi hawa kumzumea hata kabla ya kuanza kusikiliza kero zao, hali hii inalilazimu jeshi la polisi kutuma askari wake kulinda usalama shuleni hapo kwa siku ya tatu leo huku uongozi wa shule hiyo ukiendelea kuwasiliana na serikali juu ya yale yanayoendelea shuleni hapo ,na hatimaye afisa elimu wa mkoa wariambora Nkya anakuja shuleni hapo na kisha kutoa uamuzi wa bodi ya shule na serikali.Kinyume na ilivyotarajiwa wanafunzi hao ambao awali walikuwa wakigoma kuondoka shuleni hapo ,baada ya amri ya afisa elimu huyo ,walianza kuondoka na mizigo yao ambapo tayari magari yalishafika shuleni hapo kwa kubeba wanafunzi lakini wengine walionekana hawana fedha na kulazimika kutembea kwa miguu kuomba hifadhi kwa wakazi wa morogogo wakati wakiwasiliana na, wazazi wao wawatumie nauli na hapa wanapasa sauti zao.
Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo laison Saming'o hakuonekana shuleni hapo ili kujibu tuhuma zinazomkabili na huku habari zaidi toka shuleni hapo zikielezakuwa mkuu huyo wa shule alijifungua ofisini kwake tangu juzi akihofia wanafunzi hao ambao walikuwa na ghadhabu kubwa dhidi yake na kutaka aondolewa shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment