Pages

Monday, July 29, 2013

MONALISA ACHOMOA KUOLEWA TENA.

MKONGWE kwenye soko la filamu Bongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amesema hatarajii kuolewa tena baada ya kuvunjika kwa ndoa zake ikiwemo ile ya prodyuza, George Otieno ‘Tyson’.
Yvonne Cherry ‘Monalisa’.
Akisimulia maisha yake mbele ya paparazi wetu, Monalisa alisema kuna siku walipokuwa kwenye kikao cha maandalizi ya send off ya mama yake (Suzan Lewis ‘Natasha’), alitania kwa kusema ataolewa Desemba lakini hakuwa ‘siriasi’.
“Sina mpango wa kuolewa kabisa, kwanza sina mchumba nitaolewaje? Siku ile nilikuwa natania tu kwa sasa sipo tayari kufanya tendo hilo,” alisema Monalisa.
Credit GLP

No comments:

Post a Comment