Pages

Thursday, July 25, 2013

TRENI YAUA 78, YAJERUHI ZAIDI YA 140 NCHINI HISPANIA.

Hali ilivyokuwa baada ya ajali kutokea.

Baadhi ya majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza eneo la ajali.
Vikosi vya uokoaji vikiwa kazini baada ya ajali.
Mabehewa yakiondolewa kutoka eneo la ajali.
Zoezi la uokoaji likiendelea.
(PICHA ZOTE NA REUTERS)
TRENI ya abiria imeua takribani watu 78 na kujeruhi zaidi ya 140 nchini Hispania jana usiku. Katika video iliyochukuliwa na kamera za CCTV yenye sekunde 11 inaonyesha treni hiyo ikijaribu kukata kona eneo la Santiago de Compostela, Galicia Kaskazini - Magharibi mwa Hispania katika spidi kali. Lakini kabla hata haijamaliza kona hiyo, ilipata ajali mbaya kuanzia mabehewa ya mbele na kusababisha maafa hayo makubwa. Ajali hiyo imetajwa kuwa miongoni mwa ajali mbaya za treni kuwahi kutokea balani Ulaya.

Tukio hilo baada ya kunaswa na kamera hizo liliwekwa katika tovuti ya gazeti la nchini humo la  El Pais na baadaye kuwekwa katika tovuti ya YouTube.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, dereva wa treni yupo katika uchunguzi baada ya tukio hilo.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mariano Rajo, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment