Pages

Monday, July 29, 2013

Watu 480 wauawa kwenye machafuko ya Misri

Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin ya Misri imetangaza kuwa, kwa akali watu 480 wameuawa, 8,000 kujeruhiwa na wengine 1,500 kutiwa mbaroni kwenye ghasia na machafuko yaliyodumu kwa wiki tatu nchini humo. 

 Chama cha Uadilifu na Uhuru, tawi la kisiasa la Ikhwaanul Muslimiin, kimeeleza kuwa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, watu wasiopungua mia nne na themanini  wameuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa pamoja na kufungwa kanali tisa za televisheni za harakati hiyo.

 Taarifa zinasema kuwa, machafuko na mapigano nchini humo yamesababishwa na hatua ya jeshi ya kumuondoa madarakani na kumuweka kizuizini Rais Mohammad Morsi wa nchi hiyo. 

Wafuasi wa Morsi wamekuwa wakijitokeza barabarani kila siku kumuunga mkono kiongozi huyo na hivyo kukabiliwa na hatua kali za jeshi.
Chanzo: kiswahili.irib.ir

No comments:

Post a Comment