Pages

Thursday, August 29, 2013

Arsenal yafuzu makundi Ulaya

London, England.
Aaron Ramsey alifunga mara mbili na kuiwezesha Arsenal kusonga mbele kirahisi hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Fenerbahce mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia jana.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 5-0, kufuatia kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza.

Ramsey, aliyefunga bao moja kati ya matatu ambayo Gunners walishinda katika mchezo wa kwanza ili iliyopita nchini Uturuku, alifunga bao la kwanza dakika ya 25.
Pamoja na wageni kucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza, vijana wa Kocha Arsene 

Wenger walijihakikishia ushindi kwa Ramsey kufunga bao la pili dakika ya 72.
Nayo Vienna ilikata tiketi ya kucheza hatua za makundi kufuatia ushindi wa jumla mabao 4-3 Dinamo Zagreb.
Timu inayocheza Ligi ya Bundesliga, Schalke ya Ujerumani ilishinda mabao 3-2 dhidi ya PAOK Salonika na hivyo kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Adam Szalai alikuwa wa kwanza kufunga kwa Schelke, kabla ya tefanos Athanasiadis kusawazisha, na kisha Julian Draxler kufunga bao la pili kwa Wajerumani.Dakika ya 79 Kostas Katsouranis alifunga bao la kusawazisha kwa Salonika, na kisha Zalai kufunga bao la pili.

Steaua Bucharest ilipoteza uongozi wa kufunga mabao mawili na kisha kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Legia Warsaw katika mechi iliyochezwa nchini Poland. Hata hivyo, imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
Nicolae Stanciu na Federico Piovaccari waliifungia mabao Bucherest ndani ya dakika 10.

No comments:

Post a Comment