Pages

Wednesday, August 28, 2013

BAADA YA KIMYA KIREFU, GK AIBUKA NA NGOMA MPYA.

MSANII mahiri katika anga za muziki wa Bongofleva, Gwamaka Kaihura 'King Crazy GK' leo ameibuka na singo yake mpya iitwayo Baraka au Laana aliyomshirikisha msanii Yuzo.
GK (katikati) akiwa na DJ Fetty (kushoto) na msanii Pauline Zongo (kulia) ndani ya Studio za Clouds FM leo.
GK alikuwa kimya kwa takribani miaka sita baada ya kuwa busy na masomo kitendo kilichopelekea kuupa kisogo muziki kwa muda na kuwafanya mashabiki wake kum-mis katika fani hiyo. Memba huyo wa East Coast Team ameachia ngoma yake mpya leo na anataraji kuachia video yake siku ya Ijumaa Agosti 30, mwaka huu. Akiongea na MTANDAO HUU, GK alisema kuwa amerudi kwenye game kwa nguvu zote na amewashukuru baadhi ya wadau kama Eric Shigongo, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kumtia hamasa ya kurudi kwa nguvu mpya baada ya kupotea kwa muda.

No comments:

Post a Comment