Pages

Friday, August 16, 2013

KUTOLEWA HOSPITALI SHEIKH PONDA, VIONGOZI WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU WATOA TAMKO.


Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Rajan Katimba (katikati) akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mjumbe kutoka Organization of Scholers in Tanzania, Ally Basalleh naye akiongea wakati wa mkutano huo.
Wanajumuiya hao wakinena mara baada ya mkutano huo.
Polisi wakidumisha ulinzi nje ya msikiti wa Mtambani ambapo mkutano umefanyika.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini.
Viongozi wa Dini ya Kiislamu leo wamekutana na wanahabari katika msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar, kujadili juu ya kutolewa hospitali Katibu Mkuu wa Jumuiya na  Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. Sheikh Ponda alichukuliwa na polisi kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) jana majira ya saa nne na nusu asubuhi. Katika taarifa yao waliyoitoa kwa wanahabari, viongozi hao wamelaani kitendo hicho alichofanyiwa Sheikh Ponda na kuitisha mkutano wa dharura utakaofanyika Jumapili ya Agosti 18 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Viwanja vya Nuruh Yakin Temeke jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA DENIS MTIMA / GPL)

No comments:

Post a Comment