Pages

Monday, August 19, 2013

Mengi mwenyekiti mpya bodi TPSF.

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 14 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) wamemchakua Dk. Reginald Mengi kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya taasisi hiyo.

Mengi alichaguliwa kuwa mwenyekiti katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki ukiwa ni sehemu ya mkutano mkuu wa mwaka baada ya bodi iliyokuwa ikiongozwa na Esther Mkwizu kumaliza muda wake.

Uchaguzi huo ulioendeshwa kwa njia ya kura ulisimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.

Katika uchaguzi huo, Mengi alipata kura 39 na mgombea mwingine, Salum Shamte alipata kura 34, hivyo kuwa makamu mwenyekiti wa bodi hiyo.
Mkutano huo mkuu pia uliwachagua wajumbe 11 walioomba uongozi kupitia kongano wanazotoka ili kuwa wajumbe wa bodi hiyo.

Baada ya kutangazwa mshindi, Mengi alisema katika kipindi chake atashirikiana na bodi na sekretarieti ya TPSF kuhakikisha yale yote mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita yanaendelezwa.

Alitoa changamoto kwa serikali kutumia fursa za rasirimali zilizopo nchini kwa kuwapa kipaumbele Watanzania kwa ajili ya maslahi zaidi ya nchi kama zilivyofanya nchi za Korea Kusini na Malasia.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, alisema taasisi hiyo imepata kwa mara nyingine viongozi mahiri katika nyanja ya masuala ya biashara na wenye ushawishi katika kuzungumza na serikali.

No comments:

Post a Comment