Pages

Saturday, August 31, 2013

MTITU ASHINDA VITA YA USAMBAZAJI.

BAADA ya kuwekewa vizingiti katika kazi yake ya usambazaji wa filamu, Mkurugenzi wa Kampuni ya 5 Effect, William Mtitu amesema anamshukuru Mungu kwani ameishinda vita hiyo.
Kabla ya kufanikiwa kusambaza filamu yake ya Omega iliyotoka Jumatatu iliyopita, inadaiwa kwamba kampuni moja maarufu ya usambazaji wa filamu jijini Dar ilimwekea vizingiti kwa kutoa filamu kila siku ambazo Mtitu alitangaza kuitoa kwa mara ya kwanza filamu hiyo.
 
“Najivunia kwamba nimeshinda vita maana jamaa walikuwa wakinifanyia mchezo mchafu. Kila nilipotangaza kutoa filamu na wao wakawa wanaingiza filamu mpya lakini nashukuru Mungu kwamba sasa hivi nimeweza.
 
“Huwezi kuamini, nilipoingiza sokoni Omega ndani ya masaa matano nililazimika kuongeza nakala nyingine kwani inanunuliwa kama karanga,” alisema Mtitu

No comments:

Post a Comment