Pages

Thursday, August 15, 2013

NI SAHIHI UCHAGUZI WA TFF KUFANYIKA SIKU MOJA NA MECHI YA SIMBA VS YANGA? TOA MAONI YAKO

Shirikisho la soka nchini jana limetangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi viongozi wa shirikisho hilo na bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara ambapo tarehe 20 na 18 ndio siku ambazo chaguzi hizo zinafanyika. Uchaguzi wa TFF tarehe 20 Oktoba na bodi ya ligi tarehe 18.

Lakini pia ikumbukwe ratiba ya ligi kuu msimu ujao inaonyesha kwamba mechi ya watani wa jadi ya Simba na Yanga ya raundi ya kwanza itakuwa tarehe 20 Oktoba pia siku moja na uchaguzi wa TFF.Kwa ukubwa wa matukio haya mawili kufanyika nadani ya siku moja kunahitajika kujipanga ukizingatia yanaingiliana. Tayari baadhi ya wadai wameshaanza kuonyesha wasiwasi wao kuhusu matukio haya kufanyika siku moja - mmojawapo ni aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Bwana Fredrick Mwakalekebela, je wew kama mdau una maoni gani?.

No comments:

Post a Comment