Pages

Thursday, August 1, 2013

Snura aahidi makubwa kwenye video ya ngoma yake “Nimevurugwa”


snuramajanga
Baadhi ya mashabiki wa Snura walikuja na  maoni tofauti juu ya video ya majanga, kuna waliosema kwamba kuna vitu walitegemea sana kwenye video hiyo lakini vimekuwa kidogo sana. 

Majanga ngoma ya Snura ambayo ilimuweka rasmi kwenye ramani ya muziki msanii huyu wa bongomovie na bongoflava hadi kupata nafasi ya kufanya show kwenye Kili Music awards na show nyingine kibao.

Snura amefunguka kwamba amejua nini mashabiki wake wanahitaji hadi kwenye video zake, sasa kwenye video atakayo fanya kwa ajili ya ngoma yake mpya aliyoitoa hivi sasa “Nimevurugwa”, atahakikisha mashabiki zake wanapata kile wanachokitegemea.

“Video ya Majanga ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu na nilikuwa sijajua vizuri mashabiki wangu wanataka vitu vya aina gani kwenye video. Nishafanya show nyingi ambazo zimenisaidia kujua kitu ambacho mashabiki zangu wanapenda nikiwa kwenye show. Ndiyo maana sikosei kabisa kwenye kila show ninayofanya sasa hivi. Naamini video ya Majanga imekuwa somo kwangu na nitafanya poa kwenye video ya Nimevurugwa na nyingine zote zitakazo kuja”

No comments:

Post a Comment