Pages

Wednesday, August 14, 2013

Uchaguzi TFF hadharani leo

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo inatarajiwa kutangaza rasmi mchakato wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Hamidu Mbwezeleni, leo atazungumza na waandishi wa habari kuelezea mchakato utakavyokuwa, ikiwamo tarehe mpya ya uchaguzi huo.

“Uchaguzi huo awali ulikuwa ufanyike Septemba 29, lakini kutokana na sheria mpya za uchaguzi zinazotaka kuwe na siku 60 toka tangazo la kuanza kwa mchakato, basi kamati itatangaza tarehe mpya ili kukidhi matakwa ya sheria hiyo mpya,” alisema Wambura.

Alisema Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Agosti 11 na kisha kikao kingine Agosti 12, ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili maandalizi ya uchaguzi huo.
Mbali ya Mbwezeleni, Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.

Wakati huohuo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, chini ya mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, jana ilianza mchakato kupitia usajili wa wachezaji wenye matatizo, kikao kinachotarajiwa kuhitimishwa leo na kutangazwa matokeo.

No comments:

Post a Comment