Pages

Friday, August 23, 2013

Wakazi Wazo wakubali uhakiki.

KAMATI ya wananchi waliokombolewa maeneo yao kutoka kwa wavamizi yaliyoko Jimbo la Kawe, imekubali Kampuni ya SKOL kuanza uhakiki wa maeneo yao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seif Mahungu, alisema kampuni hiyo itafanya kazi chini ya usimamizi wa Manispaa ya Kinondoni, hivyo kuwahimiza wamiliki wote kuhakikisha wanajitokeza wakati zoezi hilo litakapoanza.

“Kamati yetu tuliiunda kwa wananchi tuliokomboa maeneo yetu kutoka kwa wavamizi katika maeneo ya Boko, Nakalekwa, Madale, Nakasangwe, Kinondo na Mabwepande…tulikutana na kampuni hiyo jana na imetuhakikishia ipo tayari kuanza kazi hiyo chini ya usimamizi wa Manispaa,” alisema.

Alisema wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa wamiliki wa maeneo hayo Agosti 24, mwaka huu katika eneo la Wazo Polisi na kutaka kila mmiliki kufika na vielelezo kamili.

No comments:

Post a Comment