Pages

Saturday, August 24, 2013

Walter Chilambo amemshangaa mwenzake Nay Wamitego kuazisha malumbano ya kijinga dhidi yake.

MSANII wa Bongo fleva na mshindi wa BSS mwaka jana, Walter Chilambo, amemshangaa mwenzake Nay Wamitego kuazisha malumbano ya kijinga dhidi yake ili kujipatia umaarufu.

Chilambo aliyasema hayo jana alipozungumza akisema msanii huyo amekuwa na fikra finyu kuwa mafanikio ni kumiliki gari.

“Jamaa amezungumza vitu asivyovijua, amekurupuka pasipo kujua na kwanza hajavifiria kichwani na kuwa mwanamuziki sio lazima kuwa awe na gari,” alisema Chilambo.

Chilambo ametoa ushauri wa bure kwa msanii mwenzake kusugua kichwa kwani kuna vingi vya kuimba badala ya kuishia kuwaimba watu moja kwa moja kwani huo sio usanii.

“Kuna vitu vingi vya kuimba vinavyoweza kuwa na tija kwa taifa, badala ya kuimba majungu, naamini Nay hayajui kwa undani maisha yangu, hajua hata ninapoishi,” alisema.

Alipoulizwa kama anafikiria kumshtaki au kumjibu kwa wimbo, Chilambo alisema yote mawili hayana tija kwake wala kwa muziki.

‘Mimi siko kiushindani zaidi, nawaza kutoa wimbo ambao utawagusa mashabiki wangu ili nami nipate fedha badala ya kazi ya majungu,” alisema Chilambo.

Alipofuatwa Mkurugenzi wa Bechmark Production Ltd, Madam Ritha Poulsen, aliyetajwa kwenye wimbo huo kuashiria kuna yaliyojificha nyuma ya zawadi za washindi, alisema hakuna hila wala agenda ya siri kwenye suala la zawadi.

‘Mimi sina ajenda ya siri. Namtakia kila la heri, naamini yeye (Nay) ni mhangaikaji, anayejaribu kutumia jina letu kutoka,” alisema Ritha.

Majibu ya Rita ni baada ya Nay kuwashutumu kupitia wimbo akidai waandaji wa BSS wana ajenda ya siri, baada ya msanii waliyemuibua kuishi maisha ya ufukara akiwa hana hata gari wala baiskeli.

No comments:

Post a Comment