AFRICAN STARS "Twanga Pepeta" si kweli Maseneta wa bendi yetu hawatembei na Ma - dancers wetu.
Kupitia page yao ya Facebook Utawala wa Bendi ya AFRICAN STARS "Twanga Pepeta" wamekanusha yafuatayo.
TAARIFA
TOKA ASET. Utawala wa Bendi ya AFRICAN STARS "Twanga Pepeta" unapenda
kupinga shutuma zilizotolewa na admin wa Group la CHEZA KIDANSI, Bernard
James, kwamba Maseneta wa Twanga Pepeta wana tabia ya kutembea na
ma-dancers wa bend (Wacheza Shoo)i.
Habari hizo ni za udhalilishaji na
za upotoshaji.
Hivyo basi tunachukua fursa hii kuwaomba radhi Wadau wetu
wakubwa MASENETA kwa kuwa tunaheshimu mchango wao na pia ikumbukwe kuwa
hawa ni watu wazima wenye Heshima zao na wana familia zao pia.
Haipendezi tukaandika vitu vya Kuwadhalilisha watu wazima bila kuwa na
Ushahidi.
Tunaomba kuchukua Fursa hii kutamka kuwa Jambo hilo halina
Ukweli na TUNAMTAKA Mtoa taarifa hizo Akanushe au athibitishe kwakuwa
MASENETA wetu hawajapendezwa na Jambo hilo la upotoshaji usiofundisha.
No comments:
Post a Comment