Pages

Sunday, September 1, 2013

HIVI NDIVYO MWILI WA ASKOFU MOSES KULOLA ULIVYOAGWA JIJINI DAR.


Pikipiki iliyoongoza msafara ikiwasili viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke.
 VILIO vilitawala viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke jana wakati mwili wa mwasisi wa makanisa ya kiroho na mhubiri wa kimataifa,  Dk. Moses Kulola, ulipokuwa ukiagwa kwa ajili ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika mkoani Mwanza wiki ijayo.
Gari lililobeba mwili wa marehemu.
Maaskofu na wachungaji wakiwa wamejipanga kuupokea mwili huo.
Mke wa marehemu, Elizabeth Kulola (wa kwanza kulia) na ndugu wengine (kushoto) wakilia kwa uchungu.
Wajukuu wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni. Katikati ni mwimbaji wa Injili ambaye ni mjukuu wa Kulola, Flora Mbasha akilia.

Watu waliohudhuria viwanjani hapo wakilia baada ya mwili kuwasili.
Jeneza la mwili wa marehemu likiwa mbele ya waombolezaji.
Mtumishi wa Mungu, mchungaji Katunzi akitoa neno fupi na kuombea sadaka.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso,  akisaini  kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais, Gharib Bilal (wa pili kulia), akiingia viwanjani hapo.
  …Akisaini kitabu cha maombolezo.
Mchungaji, Anthony Lusekelo akisaini kitabu cha maombolezo.
Mama Getruda Lwakatare  akisaini kitabu cha maombolezo.
Askofu wa makanisa ya Pentekoste nchini, David Mwasota, akitoa neno la salamu na jinsi alivyokuwa akimfahamu marehemu Kulola.
Mchungaji Josephat Gwajima akitoa salamu za rambirambi.
(Stori/Picha: Gladness Mallya na Haruni Sanchawa /GPL)

No comments:

Post a Comment