Pages

Friday, September 6, 2013

Mahakama yamuondoa Dhaira Simba SC

Kipa wa Simba, Abel Dhaira.
KIPA namba moja wa Simba, Abel Dhaira amelazimika kuiacha klabu yake na kurudi kwao Uganda, baada ya kuitwa haraka na mahakama ya nchini humo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia Dhaira ambaye kwa sasa ndiye kipa muhimu katika kikosi hicho, kutoonekana katika mazoezi ya siku mbili ya kikosi hicho, huku kukiwa na taarifa zinazokinzana kuwa kipa huyo anaumwa.
 
Mmoja wa viongozi wazito wa Simba ameliambia Championi Ijumaa kuwa, kipa huyo amelazimika kurudi Uganda kufuatia kukabiliwa na kesi inayomhusisha kununua kiwanja ambacho tayari kilishauzwa kwa mtu mwingine.

Bosi huyo, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema Dhaira alishaomba ruhusa hiyo muda mrefu lakini msisitizo juu ya hilo ulikuja kumtaka kipa huyo kuwasili haraka kushughulikia kesi hiyo ya kiwanja kilichopo katika Mji wa Jinja nchini Uganda.
 
“Alikuwa akiomba ruhusa muda mrefu, naona sasa atakuwa ameshakwenda huko kutokana na kuitwa haraka kufuatilia kesi hiyo, kesi yenyewe imetokana na Dhaira kununua kiwanja eneo la Jinja lakini baada ya kununua akapata taarifa kuwa kiwanja hicho tayari kilishauzwa kwa mtu mwingine, wakashindwa kuelewana na ikafunguliwa kesi, sasa ndiyo amekwenda huko,” alisema bosi huyo.
CREDIT GLP

No comments:

Post a Comment