Pages

Monday, September 16, 2013

NISHA AWAPIGA TAFU CHIPUKIZI

Nisha Jabu akijitambulisha na kuwasalimia wasanii chipukizi waliojitokeza katika usahili.
Wasanii mbalimbali waliojitokeza wakiandika majina.
Wastara Juma (aliyesimama) akijitambulisha na kuwasalimia wasanii.

Wasanii chipukizi wakifanya majaribio ya kuigiza.
Baadhi ya majaji wakijadiliana jambo, Nisha (kushoto), Wastara (katikati) na Benny Kinyaiya (kulia).

MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ jana aliendesha zoezi la kuwafanyia usahili wasanii chipukizi ambapo alikuwa akitafuta wasanii 50 kwa ajili ya kufanya nao kazi katika kampuni yake ya Nisha’s Film Production.
 
Zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa Vijana, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo majaji waliokuwa wakiwafanyia usahili wasanii hao ni, Wastara Juma, Idrisa Makupa ‘Kupa’ Jimmy Mafufu, Benny Kinyaiya na Nisha mwenyewe.
(Habari / Picha: Na Gladness Mallya / GPL)

No comments:

Post a Comment