Pages

Wednesday, September 18, 2013

Redd’s Miss Tanzania waaswa kuthamini vya nyumbani.

WAREMBO wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries (TDL), David Mgwassa, wakati akizungumza na warembo waliotembelea kiwanda hicho kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

“Nyinyi ni mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa za humu ndani, hivyo nawaomba sana mzipende na kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda vya ndani,” alisema Mgwassa.

Alisema kuwa TDL kupitia kinywaji cha Zanzi, imeamua kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa sh milioni 40, lengo likiwa kukitangaza kinywaji hicho, pia kuboresha shindano hilo.
 
Mgwassa alisema shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa taifa na kuwataka warembo hao kutangaza vivutio vya utalii nchini kama Mlima Kilimanjaro, sambamba na kukitangaza kinywaji cha Zanzi kuwa ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Septemba 21, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment