Pages

Wednesday, September 11, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 IRINGA NGOMA INOGILE.


Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyokwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
  Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.
 Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake  kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta  linafanyika usiku huu.
Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
 Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba jukwaaniwakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora. 
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Samora.
  Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga.
 Ni noma saana
Anaitwa Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma kila kona ya uwanja.
 Anajiita Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mmoja wa madansa machachari sana kutoka THT,aitwaye Msami akiwa amebebwa juu na mashabiki baada ya kuonesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jukwaani.
Wasanii wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja.

No comments:

Post a Comment