Pages

Sunday, September 8, 2013

Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Gambia

TANZANIA, Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Gambia usiku  kwenye Uwanja wa Independence mjini Banjul katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kuhitimisha hatua ya awali ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.   
Mbaya wetu; Mustafa Jaju amefunga
mabao yote ya Gambia
Kwa matokeo hayo, Stars imemaliza na pointi sita katika nafasi ya tatu, nyuma ya Morocco wa pili na Ivory Coast vinara wa kundi, wakati Gambia wameshika mkia kwa pointi zao nne, huu wa leo ukiwa ushindi wao pekee kwenye kundi hilo.   
Stars imechapwa 2-0 Gambia
Mbaya wa Stars leo alikuwa ni mshambuliaji Mustapha Alasan Jarju mwenye umri wa miaka 27 aliyefunga katika dakika ya 45 na 51 mabao yote hayo. Mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Morocco na Tembo wa Ivory Coast unaendelea kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, Simba wa Atlasi wakiwa wanaongoza 1-0 dakika za lala salama, lililofungwa na Youssef El-Arabi dakika ya 53.
Amechemsha; Stars imeshindwa kupata mafanikio chini ya Kim Poulsen
Matokeo haya yanaamisha kufeli vibaya kocha Mdenmark, Kim Pouslen baada ya awali Tanzania kukosa tiketi za kucheza Fainali za AFCON na CHAN chini yake. Kim alirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen Mei mwaka jana na leo ulikuwa mchezo wake wa 16 kazini, akifungwa saba, sare nne na kushinda mitano.   Kikosi cha Gambia kilikuwa; B. Sanyang, A. Mansally, O. Colley, S. Marreh, T. Jaiteh, E. Sohna, H. Barry, S. Faal, M. Jarju na M. Ceesay. Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni/David Luhende dk 70, Vincent Barnabas, Mrisho Ngassa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Amri Kiemba, Khamis Mcha ‘Vialli’/Jum a Luizio dk 61, Haroun Chanongo, Frank Domayo na Simon Msuva.
Credit to BIN ZUBERY BLOG

No comments:

Post a Comment