Pages

Thursday, September 12, 2013

Usalama wa abiria bandarini bado tete

Wakati Wanzibari wakiadhimisha miaka miwili tangu kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islanders, imeelezwa kuwa uingiaji na utokaji wa abiria katika vyombo vya usafiri katika Bandari ya Malindi, si salama.

Hayao yametanabahishwa na washiriki wa kongamano la kumbukumbu ya kuzama kwa meli hiyo.
Ofisa Mwaadamizi wa Kampuni ya Azam Marine, Abdulrazak Shan Ismail, alisema udhibiti wa abiria wanaoingia na kutoka katika vyombo vya usafiri katika bandari hiyo, unapaswa kuangaliwa upya.

Abdulrazak alisema kukosekana kwa umakini katika sehumu ya kutokea magari yanayotuimiwa na abiria kuingia na kutoka, kunahataraisha usalama wao. (Mwinyi Sadallah)

No comments:

Post a Comment