Pages

Sunday, September 29, 2013

YANGA YAICHAPA 1-0 RUVU SHOOTING SIKU YA JANA.


Hamis Kiiza (20) akishangilia bao alilofunga dhidi ya Ruvu Shooting leo pamoja na Kavumbagu, Niyonzima, Msuva na Chuji






















Young Africans Siku ya jana imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho ilipoteza kwa kufungwa na Azam FC mabao 3-2 iliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo huo na ndivyo ilivyokua.

Ikiwatumia washambuliaji wake Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Mrisho Ngassa, Young Africans ilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa timu ya Ruvu Shooting lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake kuliiinyima bao la mapema.

Dakika ya 27, Saimon Msuva alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga akiwa yeye na mlinda mlango Abdu Juma Seif huku Hamis Kiiza pia akishindwa kutumia nafasi kama hiyo dakika ya 33 ya mchezo.

Washambuliaji wa Ruvu Shooting  walifanya mashambulizi langoni mwa goli la Yanga kupitia kwa Cosmas Lewis, Jerome Lembele na Elias Maguli lakini umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa kikwazo kwao kuweza kuziona nyavu za Ally Mustapha 'Barthez'.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 1-0 Ruvu Shooting.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Athuman Idd 'Chuji aliyechukua nafasi ya Frank Domayo mabadiliko yaliyopeleka watoto wa Jangwani kuutawala mchezo katika sehemu ya kiungo.

Dakika ya 63 mshambuliaji Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao la kwanza na la ushindi baada ya kuitumia vizuri krosi ya Mrisho Ngassa aliyemtoka mlinzi Stephano Mwasika na kupiga krosi iliyomkuta mfugaji aliyefunga bao hilo maridadi na la msimu. 

Mara baada ya bao hilo Yanga iliendelea kufanya mashambulizi langoni mwa Ruvu Shooting lakini mpira uliopigwa na Didier Kavumbagu uliokolewa na golikipa Abdul Juma Seif na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1- 0 Ruvu Shooting.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernie Brandts amesema anashukuru vijana wake wamepigana kuhakikisha wanapata ushindi katiika mchezo wa jana, ukizingatia timu ilikua imetoka kupoteza mchezo wake wa mwisho.

Ushindi huu wana Yanga wote, tunaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumamosi ijayo. 

Young Africans: Mustapha, Twite, Luhende, Yondani, Nadir, Domayo/Chuji, Msuva.Nizar, Niyonzima, Kavumbagu, Kiiza, Ngassa

No comments:

Post a Comment