Pages

Wednesday, October 9, 2013

Mama Lishe ajishindia nyumba ya Airtel.

MAMA Lishe, Husnut Anthony John, ameibuka mshindi wa nyumba ya kisasa iliyoko Kigamboni jijini Dar es Salaam katika droo ya mwisho ya Promosheni ya Airtel Yatosha.

Akizungumza wakati wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam juzi, Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga, alisema mshindi huyo ni wa mwisho katika promosheni ya nyumba.

Aliwashukuru wateja walioshiriki na walioshinda huku akiwataka wateja wote kuendelea kufurahia huduma ya Airtel yenye vifurushi vya bei nafuu.

Akizungumzia ushindi wake, Mama Lishe huyo alisema hakutarajia kama angeshinda katika promosheni hiyo.

Airtel Yatosha Shinda Nyumba, ilizinduliwa Julai 5, mwaka huu na kudumu kwa siku 90.
Wakati wa promosheni hiyo, Airtel imetumia zaidi ya sh milioni 410 kwa zawadi za washindi mbalimbali.

Naye Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema huduma ya vifurushi vya Airtel Yatosha bado vinaendelea kuboreshwa, hivyo wateja waendelee kuvifurahia.

No comments:

Post a Comment