Pages

Friday, October 11, 2013

MMILIKI WA SALUTI 5 ..AWAPA CHANGAMOTO BLOGGER WA TANZANIA COPY NA PASTE SOMA HAPA.

Said Mdoe ni mmiliki wa Screen Masters na  Saluti 5 mtandao wa habari za Burudani siku ya jana Amesema "Niliwahi kusema hapo kabla, hizi copy na paste za blogs zetu ni balaa. Uzushi mmoja kwenye blog moja basi utatapakaa kwenye kila blog, mfano mzuri ni huu wa Penny kuugua na kukimbizwa hospitali eti kisa Diamond karudiana na Wema mbaya zaidi na picha ya ambulance wameweka, zaidi ya blog 20 zimehusika. Mwenyewe Penny kabaki anashangaa ...uzushi mtupu. Nakumbuka kuna siku ilitoka taarifa ya Obama kukatisha ziara ya mbuga za wanyama mtu mmoja akalianzisha akasema Obama afuta ziara ya tanzania mbona ilikuwa balaa, blog kibao zikaingia mkenge ...badilikeni jamani".

No comments:

Post a Comment