Pages

Saturday, November 2, 2013

MSTAHIKI MEYA ALIVYONUSURIKA MKONG’OTO


Stori: Mashaka Baltazar,Mwanza
TUKIO la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, Henry Matata, kunusurika mkong’oto kutoka kwa madiwani wa manispaa hiyo wakidai kutomtambua lilikuwa kama sinema.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri juzi (Alhamisi) asubuhi baada ya meya huyo kufungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela.

Katika kikao hicho, madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtaka meya huyo aondoke kwenye kiti wakidai kutomtambua ndipo ukaibuka mtiti wa mshikemshike nguo kuchanika.
 
Huku vita ya maneno ikiendelea, Matata aliwaamuru madiwani hao watoke nje ya ukumbi lakini wakamvimbia wakimtaka yeye ndiye atoke.

Baada ya kadhia hiyo kuwa kubwa huku madiwani hao wakisukumana wao kwa wao wakitaka kumpiga meja huyo, ndipo simu ikapigwa polisi Kirumba ili waje kutuliza hali ya hewa.
Hata hivyo, wakati askari hao wakisubiriwa ndipo vijana wenye miili mikubwa ‘mabaunsa’ waliodaiwa kuwa wapambe wa

Matata wakavamia ukumbini kumnusuru na hakuna mtu aliyekamtwa wala kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ilikuwa ni sinema ya bure huku mabaunsa wakipongezwa kwa namna walivyomuokoa meya huyo kimafia.

“Kweli kabisa mabausa wamefanya kazi  nzuri kwa  sababu hali ilikuwa mbaya sana. Kama siyo kumuondoa kimafia na kiintelijensia, wangemalizana,” alisema Antony Maduhu aliyeshuhudia kila kitu.CREDIT GPL

No comments:

Post a Comment