Pages

Saturday, November 30, 2013

MTIKISIKO BIAFRA KESHO

 
Linah Sanga.
Wasanii wakubwa Bongo, watafanya shoo kali itakayoambatana na ujumbe mahsusi kuhusu gonjwa hatari la Ukimwi, wakati wa kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi 2013.
Linah, Barnaba, Amin, Linex, Recho, Snura, Ally Nipishe, Mataluma, Kundi la Makomando na wengine wengi, wataangusha shoo kali siku hiyo katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam.
Rachel Haule ‘Recho’
Mratibu wa tamasha hilo, Paul Makonda, amesema kuwa shoo hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu hatari ambayo imeendelea kutanda dhidi ya janga hilo.

“Moja wa majukumu ya UVCCM ni kusimamia ustawi wa vijana, tunajua kwamba Ukimwi ni tishio kwa kada zote lakini vijana ni wahusika wakuu, kwa hiyo ni lazima tukumbushane katika kuhakikisha tunautokomeza kabisa ugonjwa huu,” alisema Makonda na kuongeza:
“Tuna orodha ya wasanii wazuri sana ambao wanapendwa na jamii, hawa wamekubali kushirikiana na sisi, kwa hiyo watafanya shoo nzuri, bila kusahau ujumbe kutoka kwao ambao wamewaandalia mashabiki wao kwa ajili ya siku hiyo.”
Makonda aliongeza kwamba vilevile kutakuwa na watu mbalimbali mashuhuri ambao watatoa ujumbe kwenye siku hiyo, akasisitiza kuwa ni vizuri kila mwananchi akajitokeza ili aburudike na apate ujumbe mahsusi wa kumuwezesha kujikinga na maambukizi ya Ukimwi.
“Tunasisitiza shoo hiyo haina kiingilio, yaani ni bure kabisa, watu waje kuanzia saa 6:00 mchana maana shoo kamili itaanza saa 7:00 mchaa mpaka saa 12:00 jioni. Ulinzi ni wa uhakika,” alisema Makonda.

No comments:

Post a Comment