Pages

Monday, December 23, 2013

MSANII BONGO AITWA NA MAKHIRIKHIRI

MWANAMUZIKI anayetamba na nyimbo za Kisafwa zenye asili ya Mkoa wa Mbeya, Salma Omary ‘Sister Das’ hivi karibuni alipata mwaliko wa kwenda nchini Botswana kukutana na wasanii wa kundi la Makhirikhiri linaloongozwa na Shumba Ratshega.
 
Salma Omary ‘Sister Das’.
Akiwa nchini humo, Sister Das alifanya mazungumzo na wasanii wa kundi hilo kuhusu namna ya kuuinua muziki wa asili ikiwa ni pamoja na kurekodi nao video mpya ya wimbo wake wa Avinza Zyele.
“Ni kweli nilipata mwaliko nchini Botswana kutoka kwa Kundi la Makhirikhiri ambapo tuliongea mambo mengi ya kukuza muziki wa Kiafrika na kuweza kufanya maonesho ya pamoja, pia nilirekodi nao video ya wimbo wangu mpya,” alisema Sister Das.

No comments:

Post a Comment