Pages

Thursday, December 26, 2013

TAMASHA LA KRISMASI LAFANA UWANJA WA TAIFA, JIJINI DAR

Mwimbaji wa muziki wa injili Solomon Mahlangu kutoka nchini Afrka Kusini akiimba jukwaani  kwenye uwanja wa Taifa katika tamasha kubwa la Krismas lililofanyika jijini Dar es salaam likishirikisha waimbaji wengi kutoka nchi mbalimbali za afrika wakiwemo waimbaji wa Tanzania, Mwimbaji huyo Nguli wa muziki wa njili ameonyesha uzoefu mkubwa katika kuimba tofauti na waimbaji wengine waliotangulia ukiacha Ephraim Sekereti wa Zambia, kutokana na kuimba nyimbo mbalimbali za kizuru kiingereza na kiswahili kwa ufasaha.
Waimbaji wa mwimbaji Slomon Mahlangu wakiimba jukwaani.
Mashabiki wakipigishwa saluti na mwimbaji Solomon Mahlangu.
Mashabiki wa Solomon Mhlangu wakiwa ameshikana mikono huku wakiinyanyua juu.
Mgeni rasmi Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu Uratibu wa Sera na Bunge Mh. William Lukuvi akizungumza katika tamasha hilo na kuwashukuru waimbaji wa muziki wa injili kwa kuendelea kuhubiri amani nchini lakini pia akawahakikishia kwamba serikali kitahakikisha amani iliyopo inadumu, kulia ni mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na katikati ni Ezekiel Maige Mbunge wa jimbo la Msalala hivi punde atapanda jukwaani mwimbaji nguli wa muziki huo kutoka nchini Afrika Kusini Solomon Mahlangu ili kuhitimisha tamasha hilo kwa jiji la Dar es salaam.
Mwimbaji Ephraim Sekereti akitumbuiza kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la Krismasi linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam.
Mwimbaji Ephraim Sekereti akifanya vitu vyake jukwaani kwenye uwanja wa taifa.
Mwimbaji Rose Muhando akiimba na kucheza kwa hisia mbele ya mashabiki wake.

Mwimbaji Rose Muhando akiimba na kucheza kwa hisia na kundi lake mbele ya mashabiki wake.
Mwimbaji Upendo Kirahiro akiimba jukwaani.
Mwimbaji wa muziki wa injili Boni Mwaiteje akipagawisha mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Krismas linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Taifa, katika tamash hili pia yuko mwimbaji nguli wa muziki huo kutoka nchini Afrika Kusini Solomon Mahlangu.
Mwimbaji upendo Nkone akiimba katika tamasha hilo.
PICHA ZOTE NA FULL SHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment