MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa
duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia
yoyote huwa hoi.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana
kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au
hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.
“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi
starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda
kukumbatiwa.”
No comments:
Post a Comment